GET /api/v0.1/hansard/entries/937923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 937923,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937923/?format=api",
    "text_counter": 71,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Cherangany, JP",
    "speaker_title": "Hon. Joshua Kutuny",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Ijapokuwa ninaunga mkono Hoja hii, nina masikitiko kwamba ni Mbunge aliyeileta tuijadili. Tunajadili Hoja ambayo tutaizungumzia hapa lakini kutekelezwa kwake kutafanya tubaki na maruweruwe ya mazungumzo yetu hapa. Ninapotafakari na kufikiria, ninarudishwa nyuma na taswira ya mwaka wa 2013 tukiomba kura ya kuiandaa Serikali hii. Tulitoa ahadi kwa Wakenya kwamba kila mkulima atasajiliwa iwe ni mkulima wa mahindi, ngano, maziwa, au ng’ombe. Sasa ni miaka saba na hakuna mkulima aliyesajiliwa. Waswahili wanasema: “Heri nusu shari kuliko shari kamili”. Hii Hoja inatupa nafasi ya kutathmini, kuzungumzia matatizo, manufaa ya wakulima na wakulima kusajiliwa. Serikali huagiza pemebejeo za ukulima kama vile mbolea na mbegu za aina tofauti. Lakini, Serikali huziagiza ikizingatia nini au idadi ipi ya wakulima ikiwa sajili haipo? Serikali itajuaje wakulima wa mahindi ni wangapi na matarajio ya gunia za mahindi zitakazovunwa ni ngapi? Kwa sababu Serikali haina idadi kamili, isemapo kuna upungufu wa chakula katika taifa la Kenya, hapo ndipo mwanya wa matapeli hupatikana. Serikali husema tuagize vyakula ilihali taifa inaweza kujilisha. Ninashukuru na ninaweza kuripoti kwa furaha kwamba tulipinga uagizaji wa mahindi kutoka nje. Ijapokuwa mpaka sasa Serikali haijatangaza bei ya mahindi, tuna bei nadhifu katika soko. Wakulima kwa sasa wanafurahia. Vile vile, tunatarajia Serikali itangaze bei ya mahindi kwa sasa. Wakulima wanaendelea na uvunaji lakini hali ya anga si nzuri. Hi ndio sababu tunasikia mazungumzo ya aflatoxin. Baada ya vyakula kuvunwa, mbinu za kuzihifadhi zimekuwa changamoto katika taifa la Kenya. Ninapochangia Hoja hii ya kuorodhesha wakulima, niliona mojawapo ya vyombo vya habari ikiendesha kipindi kilichoeleza kuwa vyakula tunavyotumia kwa sasa ni hatari. Nakubaliana na kipindi hicho. Leo vyombo vya habari vinatueleza kuwa mahindi tunayotumia ina sumu, wali tunaoula Kenya una sumu na maziwa wanayotumia Wakenya ina sumu. Ni kipi kingine bora au kilichosalia kuwa safi nchini Kenya? Suluhu ni nini? Tunaelezwa kuwa vyakula vyote katika taifa la Kenya vina hatari, lakini hawatupei suluhu. Taarifa hii ndiyo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}