GET /api/v0.1/hansard/entries/937924/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 937924,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/937924/?format=api",
"text_counter": 72,
"type": "speech",
"speaker_name": "Cherangany, JP",
"speaker_title": "Hon. Joshua Kutuny",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "inayoendelezwa. Tunataka Serikali itoe taarifa kuhusu hili swala linalozungumziwa katika vyombo vya habari kuwa vyakula vyote vitumiwavyo na Wakenya vina makali ya sumu. Ni hatari kwa kutotoa msimamo wake juu ya swala hili. Asilimia 95 ya Wakenya wanatumia mahindi na maziwa. Wanakula sima na kukunywa chai ya maziwa. Hivi ndivyo vyakula vinavyotumiwa na watoto wote wachanga wanaozaliwa. Tunaruhusu taarifa za vitisho kuhusu vyakula vya Kenya. Katika soko la kimataifa, watu wanashuku vyakula tunavyotumia. Hawawezi kuviagiza na hatuwezi kuviuza nje ya nchi. Mbona Serikali inaruhusu habari hizo ziendelee kuzungumzwa badala ya kutupa suluhu ya kudumu? Wakulima wa majani chai wanalalamika. Kama kungekuwa na idadi kamili ya wakulima, ninaamini Kenya Tea Development Agency (KTDA) wana nafasi bora na ratiba ya kujua ni wakulima wangapi wako nao. Leo tunaangalia kwa huzuni wakulima waking’oa majani chai. Nchi itaelekea wapi? Uti wa mgongo wa taifa la Kenya ni kilimo lakini kujitolea kwa Serikali kumsaidia mkulima ni duni. Haijalishi wanajenga barabara kiwango gani wakati mkulima anahangaika. Watu hawatakula barabara. Watahitaji dawa nyingi. Hata tukifanya nini, tusipomsaidia mkulima itakuwa ni matatizo tunaingiza katika taifa letu. Mkulima akilima na kuuza mazao yake, akipewa nafasi atampeleka mtoto wake shuleni, atatafuta matibabu bora, atajiendeleza kimaisha na atajenga nyumba safi. Kwa hivyo, ninapounga Hoja hii mkono, ninataka kuisuta Serikali kwamba wamezipa kisogo zile ahadi walizowapatia Wakenya. Na hata ni juzi tu. Wakulima walikuwa wameelezwa kwamba utakapoingia kwenye shamba, kabla hujalima kile ambacho utalima, utakuwa umetangaziwa bei ndio ujue utafanya biashara ya kilimo ama utafanya biashara ya kujinufaisha na kujitosheleza. Lakini yote hayakupewa kipaumbele. Kwa hivyo, mimi ninaungana na wenzangu hapa kusema kwamba suala hili ni muhimu, lakini ni lazima tuibadilishe ikuwe sheria ndio ikuwe ni lazima mkulima asajiliwe. Asante. Nashukuru."
}