GET /api/v0.1/hansard/entries/938011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938011/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia huu Mswada. Mwanzo namshukuru Mhe. Kamket kwa kuleta huu Mswada. Mwenyezi Mungu atakubariki. Ningependa kuwaelezea Wabunge wenzangu kwamba huu Mswada ni muhimu kwa sababu kuna watu wengi wanateseka huko ndani ndani. Tusiwe sisi Wabunge ndiyo sababu ya wao kuteseka. Kama mwenzetu alivyosema, sisi wengine tumezaliwa katika haya maeneo ambayo yametengwa. Si kuchagua kwetu; ni kwa sababu ya mipango ya Mwenyezi Mungu. Leo nitazungumza kwa kihemko. Kwa wale hawaelewi Kiswahili, labda nitasema niko emotional kwa sababu nimetoka Lamu jana. Kwa bahati nzuri, tumetoka maeneo ya Kiangwi ambayo ipo Wadi ya Basuba. Iko ndani ya Msitu wa Boni. Kabla niwaeleze yale niliyoyaona kule – ambayo yatawasikitisha – tukipitisha Mswada huu, utasaidia haya maeneo. Mwanzo ni muhimu tuunge Mswada huu mkono ili mambo yaende vizuri. Vile ilivyo, wengine wametengezewa barabara na kupelekewa maji. Tunasaidia lakini hatumalizi hizo shida. Kuna vijiji vilivyo na shida ya kutokuwa na hivi vitu vyote kama vile maji na elimu. Ningeomba wahusika, ikiwezekana, wachague vijiji ambavyo vimeathirika kabisa nchini ili visiseme vimetengwa. Kuna vijiji vidogo kama Kiangwi vyenye matatizo yote hapa duniani. Tuzisaidie mpaka ionekane kwamba tumeziinua ili siku zijazo ziwe zimepiga hatua nyingine. Wenzangu wamechangia elimu. Ningependa kushukuru Wizara za Elimu na Usalama. Kwa miaka mitano, shule za Kiangwi na Basuba zimefungwa. Jumatatu ya wiki hii, tumekwenda na tukakubaliana shule hizo zifunguliwe baada ya mimi kufuatilia na kupiga kelele. Nashukuru maana walisema shule zote zitafunguliwa baada ya miaka mitano. Hakuna Mbunge yeyote ambaye sehemu yake shule zimefungwa hata kwa mwaka mmoja. Tukizungumza kuhusu kutengwa, tunajua tunazungumza nini. Hatujipendekezi tu. Ni baada ya miaka mitano shule hizi zinaenda kufunguliwa. Nashukuru wamefanya hivyo. Nilikuwa na wenzetu kutoka idara mbali mbali tulipoenda kujionea mambo ya pale Kiangwi. Tulipokuwa kule, kuna mmoja wa wahudumu wa Kenya Red Cross amabaye katika mazungumzo yake, aliwaambia watu wa Kiangwi kuwa kwa sasa mvua inanyesha, wahakikishe wameficha vyeti vyao vya kuzaliwa hata ikiwa watazipeleka kwa majirani wao ili zisinyeshewe. Usemi kama huu, utakueleza hali ilivyo. Watu walio kule wananyeshewa kutokana na shida zilizoko. Ni vizuri sisi kama Bunge tupange Wabunge watembee waone zile hali. Tulipoenda kama kamati Lamu, tuliaambiwa mbona tunasema tumetengwa na Lamu"
}