GET /api/v0.1/hansard/entries/938016/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938016,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938016/?format=api",
    "text_counter": 164,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "zote. Kwa mfano, kuna watu wanaofanya kazi kwa Jeshi. Kwa hivyo, wanaofanya kazi kule wana matatizo mengi kwa sababu ya ukosefu wa vitu kama barabara, maji na hospitali. Wanaofanya kazi kule ni wenu pia; wateteeni maana wanapoenda kule, pia wao wanapata shida hizo. Nilienda kuona Jeshi kule. Wana shida. Zile sehemu ni ngumu. Ukienda kuwaona askari wanaokaa kule na kulipwa sawa na walio kwingineko, pia nao wanapata shida. Kuna sheria zimewekwa kwamba, walimu wapelekwe kokote kwa sababu Serikali inataka tujumuike pamoja kama Wakenya. Walimu wakitolewa Lamu kupelekwa sehemu zingine, imekuwa sawa. Lakini wa sehemu zingine wakipelekwa Lamu, wanakimbia. Hawawezi kuishi katika yale mazingira. Tunaomba serikali inapopanga policies, sehemu kama Lamu iangaliwe. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ukiniruhusu, hiyo delocalisation haifanyiki Lamu ingawa inalazimishwa. Sisi, wakati mwingine, tunaenda extra mile kusomesha wanafunzi wa kule Kiangwe ili waweze kufundisha sehemu yao ya Waboni na pakitokea shida, wasikimbie. Utapata kuwa wale waliokubali tukawasomesha, hukubali kuchukuliwa kupelekwa sehemu zingine ilhali wengine wakipelekwa Kiangwe, hawataki kwenda. Sera hii ni nzuri lakini haiwezi kutekelezwa Lamu. Tunataka tufikiriwe katika swala hili. Nimelalamika kuwa walimu wameandikwa lakini wanapelekwa kaunti jirani na wale wa county jirani wanaletwa kwetu. Watafanya kazi kivipi na shida ya Boni imekuwepo kwa miaka mitano? Ukiwaleta walimu, watakimbia na shida zetu zitasalia kuwa vile vile. Kwa hivyo, kabla ya sheria hii kupitishwa, watufikirie maana kila wanapobandika sheria hizi kwa nguvu na hazitekelezeki, wanazidi kutusukuma chini. Ninaunga mkono Mswada huu na ninaomba Mhe. Kamaket na Waheshimiwa wenzangu watuunge mkono. Kama hamuamini ninayosema, naomba mtembee Basuba Ward mujionee; mtalia. Sizungumzi kuhusu sehemu zingine za Lamu. Watu hawana hata nguo za kuvaa. Sasa nina mobilise nipate manguo nipeleke kule. Sikatai kuwafanyia haya lakini hatuna ule uwezo wa kuwafanyia haya. Ahsante."
}