GET /api/v0.1/hansard/entries/938048/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 938048,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938048/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ganze, ODM",
"speaker_title": "Hon. Teddy Mwambire",
"speaker": {
"id": 13334,
"legal_name": "Teddy Ngumbao Mwambire",
"slug": "teddy-ngumbao-mwambire-2"
},
"content": " Asante sana, Bwana Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Mswada ulio mbele ya Bunge. Nina tashwishi kama vile mwenzangu kutoka Eneo Bunge la Kilifi Kaskazini alivyosema kwamba mpango huu unaonekana kuwa mzuri. Uhaba wake ni kwamba zile sehemu ambazo zimeongezewa hazitaweza kuleta ufanisi ama maendeleo kamilifu kama vile tungependelea. Eneo Bunge ninalowakilisha kule Kaunti ya Kilifi ndilo eneo bunge maskini zaidi. Katika mwaka wa 2013, lilinukuliwa kama eneo bunge maskini zaidi hapa Kenya. Hatujaona nukuu nyingine ambayo imelitoa katika sehemu hiyo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}