GET /api/v0.1/hansard/entries/938049/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 938049,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938049/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ganze, ODM",
"speaker_title": "Hon. Teddy Mwambire",
"speaker": {
"id": 13334,
"legal_name": "Teddy Ngumbao Mwambire",
"slug": "teddy-ngumbao-mwambire-2"
},
"content": "Nashangaa kwa sababu katika ule muda ambao tumekuwa na hizi Pesa za Usawazishaji wa Maendeleo, hatujapata pesa ambazo zinaweza kutusaidia zaidi. Zimekuwa zikipelekwa katika kaunti ama serikali-gatuzi kuangalia maeneo yale. Kwa sababu kulikuwa hakuna mwelekeo thabiti au maalumu, umefanya maendeleo yaenezwe katika maeneo bunge ambayo hayajaathirika sana. Kuna umuhimu wa kuangalia huu mfumo mpya ili urekebishwe na kuhakikisha kuwa maeneo bunge ambayo yameathirika zaidi yanapata maendeleo yanayoambatana na vile ilivyopendekezwa katika Katiba. Kulingana na vile ambavyo mambo yalivyo kufikia leo, bado tuna matatizo makubwa. Tukiangalia ile miradi ambayo imefadhiliwa na pesa hizi hivi juzi, utaona kuwa maeneo bunge mengi - yakiwemo yale ambayo yanabashiriwa kwamba yana afueni - yalipewa senti hizi. Yamepata senti hizi kwa wingi zaidi kushinda hata yale maeneo yetu ambayo yameathirika zaidi. Hivyo basi kufikia leo, bado tuna matatizo makubwa ya kupata maji, barabara na vituo vya afya. Itakuwa vyema kama kutakuwepo na mpangilio maalum baada ya muda ili tuangalie kama tumepiga hatua ama bado tuko hivi, kuliko kupeana pesa tu kwa maeneo pasipo na kufuatilia kikamilifu. Nimeangalia eneo bunge langu na nikaona kwamba limezingatiwa kule chini kabisa kuanzia zile sub-locations . Ukiangalia, utapata kwamba kama ni kupeana pesa kuambatana na vile viegezo ambao vimewekwa, itamaanisha kwamba tutakuwa tunapata pesa kidogo zaidi. Kwa mfano, sub-location ya Mitsedzini katika eneo bunge langu ikipatiwa shilingi nusu milioni na inahitaji maji, inamaanisha wazi kwamba ule mradi wa maji hautaweza kukamilika katika maeneo hayo. Itakuwa vigumu kutoa pesa katika sehemu nyingine kupeleka kwa sehemu moja ili uweze kupata mradi ambao utakuwa kamilifu. Hivyo basi, mapendekezo yangu katika yale mabadiliko ambayo tutaleta ni kuwa pesa ziwekwe katika maeneo bunge ili maeneo ambayo yameathirika zaidi yaangaziwe na yapatiwe miradi ambayo itaambatana na lile tatizo liko ili miradi ikamilike. Hatutaki tuwe na miradi katika maeneo yetu ambayo haijakamilika au haitaleta manufaa kwa wananchi wetu. Tunataka tuhakikishe kwamba miradi yote inaleta afueni na usawa ambao unatakikana katika Katiba ili tujivunie kama Wakenya wengine na tuache kulia na kuvumilia. Tutafurahia matunda ya Uhuru na pesa za usawazishaji zisawazishe kama ilivyodhamiriwa katika Katiba."
}