GET /api/v0.1/hansard/entries/938309/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938309,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938309/?format=api",
    "text_counter": 207,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
    "speaker_title": "Mhe. Mbogo Ali",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Asante sana Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii nichangie Mswada huu muhimu. Mengi yamezungumzwa na viongozi Wabunge kuhusu suala hili, ambalo ni muhimu sana. Limewaumiza Wabunge wa zamani, wale waliotoa huduma katika Bunge hili. Walihudumia Wakenya katika nyanja tofauti tofauti. Kama tujuavyo, Mbunge akishatoka katika Bunge hili kwa njia moja au nyingine, ni vigumu kuajiriwa katika shirika lolote. Hata hivyo, tunashukuru korti zetu kwa kupitisha, juzi, ile sheria kwamba unaruhusiwa kuajiriwa au kupata kazi katika kamisheni ambazo ziko katika Jamuhuri ya Kenya, hata kama mtu ni Mbunge. Hilo limesaidia kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo, jambo muhimu ni kwamba sisi ndio adui wa Wabunge kwa sababu sisi ndio tunatengeneza sheria lakini sheria hizi zinakuja kutuumiza. Hii ni kwa sababu jambo kama hili lilistahili kuwa limeshughulikiwa miaka mingi iliyopita. Lakini leo sisi ambao tumekuja katika Bunge hili la Kumi na Mbili ndio tumepata fursa ya kulishughulikia. Nawaomba Wabunge wenzangu, kwa sababu kama tulivyoambiwa, ukiona mwenzako amenyolewa tia kichwa chako maji. Kwa hivyo, na sisi siku moja tutakuwa Wabunge wa zamani. Tutaitwa Wabune wa zamani pale nje. Tunavyojua Mbung ni kama askari, mwalimu na daktari. Ukishakuwa Mbunge, wewe ni Mbunge mpaka siku utakapotiwa kaburini. Majukumu hayakukimbii. Majukumu yanabaki palepale. Utakuwa unaalikwa na wakazi uliowahudumia kule mashinani na nyanjani kila wakati. Wao wanakutambua kama kiongozi: kukiwa na mazishi utaalikwa; kukiwa na mchango wa kanisa utaalikwa; kukiwa na mchango wa mambo ya masomo utaalikwa. Wale waliokupigia kura au uliowahudumia hawajui kama wewe huna uwezo kama uliokuwa nao wakati ulipokua Mbunge. Kwa hivyo, wanatazamia kila wakati unapohitajika utafika pale kuwahudumia."
}