GET /api/v0.1/hansard/entries/938313/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938313,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938313/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
    "speaker_title": "Mhe. Mbogo Ali",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Hesabu imefanywa hapa. Tumeambiwa Wabunge wa zamani ni kama 200. Ikiwa kila Mbunge atapewa shilingi 100,000 kwa mwezi, ni shilingi 20,000,000 kwa mwaka mmoja. Hizi ni pesa kidogo sana tukiangalia hali ya jinamizi la corruption ambalo linaendelea katika Jamuhuri ya Kenya. Pesa nyingi sana zimeibwa; pesa nyingi sana zinaliwa kila siku. Ikiwa pesa hizi zitatengwa kuwahudumia Wabunge wa zamani, zitawasaidia katika njia moja au nyingine. Tumekuwa na Wabunge wengi ambao wamepitia pale ninakotoka katika eneo la Kisauni. Wengi wamehudumu muhula mmoja. Wengi wako kule nyanjani. Kuna Mbunge ambaye ilifikia wakati hawezi kulipa kodi yake ya mwezi na ikawa ni aibu alipokuwa anatolewa na mwenye nyumba alimokuwa anaishi. Haya ni mambo ambayo ni lazima tuyahudumie. Nawaomba Wabunge wenzangu tuipitishe hii Hoja ambayo imeletwa mbele yetu kwa kishindo kikubwa. Hii Hoja si kuhusu wewe. Hoja hii si kuhusu yule Mbunge wa zamani. Hoja hii ni ya kuendelea kwa sababu sisi tutaondoka kesho na watakuja Wabunge wengine. Ni muhimu Wabunge wale waweze kuishi maisha mazuri watakapotoka katika Bunge hili wakati Mwenyezi Mungu atawajalia kwenda pale nje. Kwa hivyo, naunga Hoja hii mkono kikamilifu."
}