GET /api/v0.1/hansard/entries/938578/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 938578,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938578/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Katika kila kaunti kuna vijana ambao wanacheza, ilhali wao hawatahusishwa wakati kuna uchaguzi. Hii inaonyesha kwamba, kuna vibaraka ambao kazi yao ni baada ya pesa kupeanwa na Shirika la FIFA hawasikiki tena. Hawataki kujua vijana wetu watafaidikaje kwa michezo. Bw. Spika, Kamati ambayo imepewa jukumu kuhusu taarifa hii inafaa waangalie mambo haya kwa marefu na mapana. Wanafaaa wazingatie uchunguzi kuhusu ufisadi. Inafaa wajue kama ufisadi uko. Kama uko, waonyeshe wazi ni nani wafisadi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. Tukifanya hivyo, tutasaidia mchezo wa kandanda na vijana wetu kwa sababu michezo ndiyo kitega uchumi ambacho kinaweza kusaidia aliyesoma na yule ambaye hajasoma. Vijana wakiwa na talanta ya michezo, wanaweza kuitumia ipasavyo bila kuzuiliwa na wafisadi ambao kazi yao ni kujinufaisha na kujitajirisha. Asante."
}