GET /api/v0.1/hansard/entries/938593/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938593,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938593/?format=api",
    "text_counter": 102,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Katika serikali zote za kaunti nchini Kenya, utakuta watu wamesimama katika majengo ya kulipia hela hizo. Wengi hawakupata hela zao kwa sababu gavana ambaye alitangulia kuwapatia kandarasi hizo hayuko katika utawala wakati huu. Bw. Spika, utaona kwamba watu wengi wakilalamika, wakisema pending bills, na jambo hili limekua kidonda ndugu katika kaunti zote za Kenya. Hata katika Kaunti yangu ya Tana River, kuna watu wengi wanaodai pesa kwa kandarasi ambazo walifanyia serikali iliyotangulia. Wakati huu, Gavana ni mwingine, na jambo hili sio katika kaunti ya Tana River peke yake, bali katika Kenya nzima. Watu wanalalamika kuwa hawapati pesa zao. Bw. Spika, watu waliofanya kandarasi hizo walitumia pesa zao, na hata walikopa madeni katika benki tofauti tofauti. Hawawezi kupata pesa zao kwa sababu kaunti hazilipi. Kwa wakati huu, wale magavana walio katika mamlaka wanataka kufanya kandarasi mpya. Hizo kandarasi mpya ndizo walizopeana saa hii, na wako tayari kuzilipa. Hivyo hivyo, wanawacha zile kandarasi ambazo wanaziita pending bills . Wakati huu ni muafaka kwa Shirika la Magavana linaloitwa Council of"
}