GET /api/v0.1/hansard/entries/938597/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938597,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938597/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bwana Spika. Ninataka kujiunga na ndugu yangu, Seneta wa kaunti wa Wajir, Sen. (Dr.) Ali, kuzungumzia madeni ambayo yanadaiwa serikali za kaunti. Siongei kuhusu serikali ya kaunti fulani bali ninaongea kuhusu serikali zote za kaunti. Hizi kaunti hulipa watu wengine na hawalipi wengine ilhali wote wamefanya kandarasi ndani ya serikali za kaunti na hilo ni jambo la kusikitisha. Utapata ya kwamba, wale wanaofaidika katika hizi kaunti ni wale mabwenyenye. Wanabiashara wadogo katika kaunti ambao wanajaribu kujikimu kimaisha na biashara zao ndio wanapata taabu. Kwa hivyo, hii taarifa ni muhimu sana kwa taifa letu la Kenya kwa sababu linazungumzia swala la malipo ya kandarasi za wafanyibiashara ndani ya kaunti. Mara nyingi tunaona ufisadi katika kaunti kwa sababu hao hulipa wanabiashara wengine na wanakosa kulipa wengine. Hizo kaunti huwa hazipeani sababu ya kutokulipa bali hao wanabiashara wanaambiwa tu eti wangoje. Wanabiashara wadogo huwa wamechukua loans kutoka kwa benki ilhali kaunti zinachukua mwaka mmoja, mbili ama"
}