GET /api/v0.1/hansard/entries/938600/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938600,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938600/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bwana Spika. Ninataka kumpongeza ndugu yangu, Sen. (Dr.) Ali, wa kaunti ya Wajir, kwa kuleta hii taarifa. Yale maneno ambayo maseneta wenzangu wamezungumza ni ya haki na kweli kwa sababu magavana wamekuwa ni mtindo wa kutumia pesa kiholela wanapojua ya kwamba hawana hizo fedha katika hazina zao. Hao hupeana kandarasi mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wakidhani ya kwamba watawashawishi wananchi kuwapigia kura. Hao pia huajiri watu kiholela wakifikiria ya kwamba watu watawapigia kura. Ukweli ni kwamba, wananchi wanajua mtu ambaye wanafaa kumchagua. Rais alisema ya kwamba, magavana walipe pending bills lakini hakuna dalili ya kwamba hiyo inafanyika. Kuna haja ya kuzindua sheria ambayo itawajukumu magavana kulipa hizo pending bills kwa sababu hii ndiyo the biggest corruption . Kuna watu ambao huenda kukopa kwa duka ama benki wanapopata kandarasi. Yule mwenye duka hutarajia malipo na biashara yake huzama asipolipwa. Kwa hivyo, watu wengi huteseka wakati magavana wanakosa kulipa wanakandarasi. Hii ni kwa sababu huyo mtu ana watoto, bibi na hata jamaa ambao anawasaidia. Unapokata hiyo"
}