GET /api/v0.1/hansard/entries/938632/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 938632,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938632/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ya Senator wa Wajir, Sen. (Dr.) Abdullahi. Kwanza, ninampongeza kwa kuleta Taarifa hii Bungeni. Madeni yamekua ni donda sugu katika kaunti zetu. Hii ni kwa sababu kila kaunti ina madeni ya mamilioni ya pesa. Singependa kukosoa maelezo yaliyotolewa na Sen. Cherargei, kwamba, madeni yamebaki Kshs33 bilioni, lakini kusema ukweli, ripoti ya madeni yote ambayo yako katika kaunti iko mbele ya Kamati ya Uhasibu. Kamati hiyo imekua ikiwahoji magavana tofauti tofauti ili kuthibitisha ni pesa ngapi ambazo wanadaiwa na wananchi ambao ni wanakandarasi katika kaunti hizo. Sio kwamba hakuna sheria; sheria iko lakini tatizo ni utekelezaji. Utapata kwamba madeni mengi yanachukuliwa bila kufuata mpango wa kuweza kununua bidhaa na kuendeleza miradhi ambayo wamepania kufanya katika kaunti kutumia pesa hizo. Bw. Spika, pia utapata kwamba sheria ambayo inasema kwamba baadhi ya wanakandarasi, wawe ni akina mama, vijana na walemavu haifuatwi. Utapata kwamba wanakandarasi labda wameweka watoto wao ili waweze kuzingatia swala la vijana ama wameweka bibi zao kwa sababu ni wanawake ili waweze kupata kandarasi ile halafu wanajilipa kwanza na wanawacha wale wanakandarasi wengine ambao hawana labda mfadhili fulani ama Godfather katika kaunti ile kudai pesa zao kwa miaka na miaka, na hivyo, wanapoteza pesa zao."
}