GET /api/v0.1/hansard/entries/938634/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938634,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938634/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mabibi wamekimbia kutoka kwa nyumba nyingi kwa sababu ya madeni ambayo yamekumba familia ambazo zimepatiwa kandarasi na kaunti. Ukiangalia gazeti siku ya Jumatatu na Jumanne, utapata kwamba kurasa zaidi ya kumi zimeandikwa orodha ya watu ambao wanadaiwa na benki, ambao nyumba zao na mali yao zinauzwa kwa sababu ya kushindwa kulipa madeni kutokana na kazi ambazo wamefanyia kaunti. Swala hili pia haliathiri serikali za kaunti pekee; ulipaji wa madeni umekuwa shida hata kwa Serikali kuu. Kwa hivyo, ningeomba kwamba Kamati husika, itakapoangalia swala hili, itoe mapendekezo ya mambo ambayo tunaweza kufanya kwa haraka; hata kama itabidi Controller of Budget aombwe azuie kutuma pesa katika kaunti zile zenye madeni mengi. Tunataka jambo hili lifanyike ili wanakandarasi wetu walipwe madeni yao. Asante, Bw. Spika."
}