GET /api/v0.1/hansard/entries/938656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938656,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938656/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Lakini, Bw. Naibu Spika, ikijiri kwamba tunataka ndege za usafiri, na hali iwe nadra, itakuwa jambo la kusikitisha kuona ya kwamba wakati tukitafuta ndege ambazo pengine zitakuwa zinasafirisha watu kwa bei nafuu, lakini zinahatarisha Maisha yao. Hivyo basi, ingekuwa bora ndege hizo zipigwe marufuku kuliko kuhatarisha Maisha ya watu, hata kama ni ya watu wawili au watatu wakiwa ndani ya ndege hizo. Bw. Naibu Spika, tunaona hatari kubwa katika uwanja wetu wa ndege wa Wilson. Naunga mkono aliyoyasema Sen. Cherargei, kwamba hata hali ya ulinzi sio njema. Nikiwa mmoja wa wale wanaosafiri na ndege hizo mara kwa mara, nimeona kwamba mtu yeyote anaweza kuingia ndani ya huo uwanja wa ndege vile anavyotaka, ikiwa nia yake ni mbaya. Pengine hivi sasa tuko na bahati nzuri ya kwamba hakujakuwa na mtu mwenye nia kama hiyo. Lakini ikiwa kunakuwa na mtu atakayekuwa na nia kama hiyo,"
}