GET /api/v0.1/hansard/entries/938660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 938660,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938660/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Ndio; ndege inadunda kama mpira. Haiwezi kutambaa kisawasawa hadi isimame. Nikiwa mmoja wa wasafiri, kila siku moja au mbili zinazopita, hujiandaa kwenda nyumbani kwa kutumia ndege hizo katika uwanja wetu wa Wilson. Bw. Naibu Spika, kama nilivyosema, hivyo ndiyo ndege hizo zinavosafiri. Ndio sababu jambo hili ni la kusikitisha, kuweza kutambua ni ndege gani. Lakini kwa hivi sasa, ambavyo wananchi wanajua kwamba ni Silverstone, basi ni lazima kampuni hiyo wajikakamue. Kama wanahitaji ndege zao kuendelea kutumia uwanja huo, basi walete ndege ambazo hazitahatarisha Maisha ya watu. Kwa hivyo, naoimba Kamati yetu ya Uchukuzi ichunguze zaidi uhamasishaji wa watu wanaosafiri kwenda zao nyumbani, ili tusipoteze maisha ya Wakenya. Asante, Bwana Naibu Spika."
}