GET /api/v0.1/hansard/entries/938675/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938675,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938675/?format=api",
    "text_counter": 184,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Hii ni kwa sababu chombo kikiyumbayumba, pia aliye ndani ya chombo hicho pia huyumbayumba. Kwa hivyo, Sen. Wetangula, kile chombo nilichokuwa ndani, ambacho ni ndege, kilidunda mara mbili au tatu. Nilipomsikia rafiki yangu akielezea jinsi ndege hiyo haikumpeleka vizuri kwenye anga, nilikumbuka kuwa utakuwa unayumbayumba huko angani, na unadundadunga hapa kwa mchanga pia. Hiyo ni hatari kubwa sana. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, tunaiomba Kamati tekelezi ya Uchukuzi na Mawasiliano ifanye uchunguzi, kwa sababu ni juzi tu ambapo ndege hiyo ilitoka hapo uwanjani na ikaanguka hapo nje, na kuhatarisha maisha ya watu wengi. Kwa hivyo, ni vizuri Kamati hii iangalie vile ndege hizi zinafanya uchukuzi. Asante, Bwana Naibu Spika."
}