GET /api/v0.1/hansard/entries/938721/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938721,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938721/?format=api",
    "text_counter": 230,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Nilipata fursa ya kutembea na Kamati hii, haswa wakati huu. Pia, nilipata fursa ya kutembelea Hospitali ya Hola, na kwa kweli, kazi inayofanywa na Kamati hii ni nzito. Hii ni kwa sababu wanatembelea zahanati zote, na kuwaongea na madaktari walioko humo. Wakitoka huko, wanaenda kuandika ripoti yao kuhusu yale waliona kule. Kwa hali hiyo, hauwezi kujua mambo haya mpaka uhusike na utembee nao. Mimi sio mwanakamati wa Kamati hii, lakini nimetembea nao. Nilikuwa nao katika kaunti za Malindi, Mombasa na Tana River. Hivyo basi, nilijua kwamba kazi wanayoifanya ni ngumu, na wanastahili kuongezwa muda ili waweze kutuletea ripoti kamili kwa kina, ili tuweze kutengeza sehemu hiyo."
}