GET /api/v0.1/hansard/entries/938760/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 938760,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/938760/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuunga mkono na kuafiki Hoja ambayo imependekezwa na ndugu yetu, Sen. Olekina. Katika kizingumkuti hiki kwamba naibu wa gavana atakuwa hana mamlaka ama katika harakati ya kwamba atachukua ofisi nusu awache nusu, tunaona ya kwamba jambo hili limeleta hali ya sintofahamu. Kwa hivyo, Hoja hii ni muhumi ili iweze kufananua kamili ya kwamba kazi ya Gavana itaanza hapa na kuishia hapa na kazi ya naibu gavana itaanzia hapa na kuishia hapa. Hii ni kwa sababu wakati wa uchaguzi, hao wawili watasimama pamoja. Sheria inatumia neno “shall” kumaanisha kwamba ni lazima itekelezwe hivyo. Hii inamaaniisha ya kwamba ikiwa naibu wa gavana atakuwa ofisini na hana mushkili wowote kumzuia kuingia kwa ofisi, ataweza kuruhusiwa kuwa ofisi, wakati gavana aliye katika mamlaka yuko katika sintofahamu zake za kwamba yuko katika ofisi ama hayuko. Hivi sasa, mahakama imesema kwamba magavana fulani wasikaribie ofisi zao. Lakini tunaelewa kwamba siku hizi, hata simu ama mitandao zinaweza kutumika. Hata gavana akiwa Ulaya na mahakama imemwambia asikaribie ofisi, ikiwa naibu wa gavana hana kazi maalum ya kufanya isipokuwa kunywa chai saa nne; kuongea katika mikutano ya hadhara; kupewa gari na askari, itakuwa si haki kwa mtu wa kiwango cha naibu wa gavana kuwa kama mtu ambaye hajijui mbele ama nyuma. Kwa hivyo, tunasema kwamba Hoja hii, vile ambavyo imeletwa na mageuzi yake, iweze kupitishwa hivyo. Bw. Naibu Spika, naunga mkono."
}