GET /api/v0.1/hansard/entries/939479/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 939479,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/939479/?format=api",
"text_counter": 292,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "La msingi, Bw. Spika, ni kwamba uhuru wa Mahakama ni kiungo muhimu katika demokrasia ulimwenguni kote. Ndio maana katika kila sehemu, mahakama zinapewa uhuru wao ili kuhakikisha kwamba zinaamua haki baina ya wananchi na serikali; na pia baina ya wananchi kwa wananchi. Kwa hivyo, ni muhimu kwetu, kama Bunge la Seneti, tusisitize juu ya umuhimu wa uhuru wa mahakama. Uhuru wa mahakama uko mara mbili; kuna uhuru wa utenda kazi, ili kwamba mahakama zinapofanya kazi haziingiliwi kwa njia yoyote. Ndio maana tuko na Judicial Service Commission (JSC), ambayo inasimamia mahakama, kama vile hapa Bunge, tuko na Parliamentary Service Commission (PSC)."
}