GET /api/v0.1/hansard/entries/939486/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 939486,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/939486/?format=api",
    "text_counter": 299,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, suala la uhuru wa mahakama ni muhimu sana katika demokrasia. Hii ni kwa sababu mtu yeyote atakapopatikana na matatizo, lazima aende mahakamani ili kuhakikisha kwamba haki zake zitalindwa. Hivi sasa, Serikali imeingia katika vita dhidi ya ufisadi. Vita vile haviwezi kupigwa wakati mahakama hazina fedha na majaji wa kutosha kusimamia kesi zile. Vita dhidi ya ufisadi haviwezi kufaulu iwapo mahakama zitakuwa hazina nyumba za mahakama, na vilevile wafanya kazi kuhakikisha kwamba kazi zile zinafanyika."
}