GET /api/v0.1/hansard/entries/939690/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 939690,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/939690/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Asante sana. Kuna lugha ambayo mmoja alitumia kwamba key population. Miaka minane iliyopita, nilibahatika kwa sababu ya kazi ambayo nilikuwa naifanya dhidi ya wanaotumia madawa ya kulevya na nikapata safari ya kwenda nchi ya India. Nilipofika pale, kati ya wale waliofika huko ni watu wa NACADA. Nakumbuka nikiwapa kauli yangu. Tulipofika pale key population iliozungumziwa, tuliona misago na maghanithi katika sehemu ya India. Kwa hivyo, naomba tusifikirie kamwe kuleta watu ambao nia na madhumuni yao ni kuzungumza mambo ambayo ni ya kushusha hadhi. Watu kutoka nje ya nchi hii kuja kuzungumza mambo ya kipuuzi yenye ni kinyume na sheria ya Kenya na kinyume ya Katiba ya Kenya na muhimu zaidi, mambo ambayo ni kinyume na maadili yetu tunayoamini kama jamii na uaminifu wetu kama nchi na wananchi ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu. Ahsante sana, Mhe. Spika."
}