GET /api/v0.1/hansard/entries/940521/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 940521,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/940521/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "ukitembea sehemu zingine za nchi hii, wale wanafunzi hawajawahi kuwaona askari wetu wakiwa wamejihami jinsi walivyojihami sasa. Bw. Spika, hatusemi kwamba ni vibaya kwa askaris wetu kuwa katika shule zetu, kwa sababu kuna hili janga la watu kuvamiwa na majambazi na majangili katika sehemu nyingi za nchi. Tunachosema ni kwamba idadi iliyopelekwa katika shule zetu ni ya juu sana, na ni ya kuogofya wanafunzi wetu. Ningeisihi Kamati yetu husika ipendekeze kuwa askari pale shuleni watengewe sehemu maalum ili wasiwashtue wanafunzi wanapofanya mitihani yao. Itakuwa kheri ikiwa wengine wao watavaa mavazi ya kiraia, ili waweze kulinda wanafunzi wetu na kuimarisha usalama shuleni."
}