GET /api/v0.1/hansard/entries/940529/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 940529,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/940529/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Arifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Wetangula. Kusema ukweli, mazingira ambayo watoto wanafanyia mitihani yamebadilika sana, kwa sababu wengi wao wanatishiwa na uwepo wa polisi waliojihami, mahali ambapo hapahitajiki silaha kama hizo. Bw. Spika, mitihani imefanywa nchini hata kabla ya Uhuru, na mitihani bado itaendelea kufanyika katika siku za usoni. Lakini ufisadi ndio umesababisha mambo haya yote, na sasa watu wanaiba mitihani. Utapata kuwa watu wengine wanenda katika vyumba vya mtihani kuwafanyia wanafunzi mitihani. Matatizo yalioko hayapaswi kuwafanya wanafunzi wawe na hofu wanpoingia katika vyumba vya mitihani. Hapo awali, kabla ya shule kufanya mitihani, kulikuwa na mihadhara mingi ya kufanya maombi. Wakati mwingine, hii ilikuwa inatumika kupitisha karatasi ghushi za mitihani, na wazazi walikuwa wanalipa ili kuhakisha kuwa watoto wao wanafanya vizuri. Kupita mtihani si mwisho wa maisha, bali ni mwanzo tu wa hatua nyingine katika maisha ya binadamu. Kwa hivyo, isichukuliwe kama ni jambo la kufa na kupona. Ndio, mtihani unasidia kumsogeza mtu kwenye kiwango kingine cha masomo, lakini sio jambo la kufa na kupona. Serikali inapasa kuekeza mikakati itakayohakikisha kwamba mitihani ni salama kwa wanafunzi. Mikakati pia inafaa kuwekwa kuhakikisha kwamba wale walio na nia ya kuiba mitihani wanachukuliwa hatua za kisheria. Lakini haitakubalika kwa vituo vya mitihani kuwa viwanja vya kuwatisha wanafunzi. Asante, Bw. Spika."
}