GET /api/v0.1/hansard/entries/941543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 941543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941543/?format=api",
    "text_counter": 459,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omanga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13175,
        "legal_name": "Millicent Omanga",
        "slug": "millicent-omanga"
    },
    "content": "Nakisia kuwa Kshs7.5 trillioni. Sasa wanahitaji Kshs9 trillioni. Kwa nini hawatupi ratiba pesa hii yoyote ni nini inafaa kufanyia? Tunajua Kenya hii uporaji wa pesa unatoka kwenye bajeti. Ni kwa sababu hiyo unaona katika bajeti nyingi, kwa mfano, National Youth Sevice (NYS) tulipoteza mabilioni ya pesa. Watu hao wa NYS hadi sasa hawajashikwa na kuchukuliwa hatua yoyote. Tuna ona Serikali ikikimbizana na wachache tunaoambiwa ni wa Kshs20 milioni kama vile Gov. Sonko. Anakimbizwa kwa sababu eti Kshs20 milioni iliwekwa kwenye akaunti yake lakini tuna mabilioni ambayo yalipotea wakifanya bajeti kwenye NYS. Hadi sasa wale ambao waliokuwa kwenye vyeo na kuidhinisha hiyo pesa, hawajashikwa. Bw. Naibu Spika, niko upande wa wengi katika Bunge hili. Tumekuwa tukipigiwa simu na kulazimishwa na Kiongozi wa Walio Wengi Sen. Murkomen kwamba lazima tuunge mkono Hoja hii."
}