GET /api/v0.1/hansard/entries/941558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 941558,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941558/?format=api",
    "text_counter": 474,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omanga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13175,
        "legal_name": "Millicent Omanga",
        "slug": "millicent-omanga"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, nina huzuni sana kwamba mwezi uliyopita tumekuwa kwenye vuta nikuvute na Bunge la Kitaifa kwa sababu ya mgao wa pesa unaoenda kwenye kaunti. Tukikubalia Serikali uwezekano wa kuchukua madeni zaidi, mwaka unaokuja, tutapata pesa chache katika kaunti. Mwaka mwingine na mtondoo na mtondogoo pesa chache muno zitapelekwa mashinani. Bw. Naibu Spika, iwapo tutapitisha Hoja hii itamaanisha kwamba sisi hatutakuwa tunapigania ugatuzi na pesa nyingi ziende kwa kaunti zetu."
}