GET /api/v0.1/hansard/entries/941578/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 941578,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941578/?format=api",
"text_counter": 494,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omanga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13175,
"legal_name": "Millicent Omanga",
"slug": "millicent-omanga"
},
"content": "Siwezi kubali Seneta aiingie katikati yangu! Bw. Naibu Spika, kuipitisha Hoja hii ni kuuza nchi yetu. Tukikubali Serikali nafasi ya kukopa zaidi, inamaana kwamba tunaua ugatuzi. Iwapo kweli tunapigania ugatuzi na kusisitiza kuwa tunataka pesa nyingi ziende kwenye kaunti, halafu sasa tukisema kwamba Serikali iendelee kukopa na kaunti ziendelee kupata mgao wa pesa wa chini zaidi ya ile tumekuwa tukipigania juzi, tunamaanisha kuwa sisi si wakweli. Bw. Naibu Spika, ukimtazama Mwenyekiti alipokuwa akiwasilisha Hoja hii, alikuwa anaongea polepole sana. Hii ni kwa sababu tulikuwa na yeye kwenye Kamati, na ilikuwa kana kwamba hata yeye mwenyewe haamini anachokisema. Hii ni kwa sababu hata sauti yake haikua ile ya kawaida."
}