GET /api/v0.1/hansard/entries/941584/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 941584,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941584/?format=api",
    "text_counter": 500,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omanga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13175,
        "legal_name": "Millicent Omanga",
        "slug": "millicent-omanga"
    },
    "content": "Nimesikia, Bw. Naibu Spika. Ni kwa sababu tulipokuwa kwenye Kamati hiyo pamoja na Waziri, idara yake ya wataalamu wa maswala ya kifedha, sote tuliukataa msimamo wake. Lakini tulipotoka kule na kuenda kuandika ripoti kesho yake, wengine walibadili mawazo yao. Sikuelewa walibadili mawazo yao vipi kutoka wakati tulipokuwa nao tukielezwa, na keshoye wakati wa kuandika ripoti. Haiwezekani kuwa Serikali inakopa ili kulipa madeni mengine. Hii ni kumaanisha kuwa tunachimba shimo ambalo halina mwisho. Kusema ukweli, hii itakuwa na madhara hata kwa watoto wetu na watoto wa watoto wetu watakaokuja baadaye. Bw. Naibu Spika, napinga Hoja hii."
}