GET /api/v0.1/hansard/entries/941758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 941758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941758/?format=api",
"text_counter": 30,
"type": "speech",
"speaker_name": "Samburu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia hii nafasi ili niunge mkono Ombi la Hon. Lentoimaga. Kuna maana ya Mhe. Lentoimaga kuandika Ombi hili. Nafikiri tuko na shida kubwa sana kuhusu haya mambo ya wizi wa mifugo. Sijui kwa nini inaitwa wizi wa mifugo ilhali ni kitu inaua wananchi katika pembe zote. Vita vilivyoko Baragoi ni mbaya zaidi. Ninaomba Kamati ya Usalama ichukue hatua na ihakikishe Waziri wa Usalama awe hapa ili wakutane. Shida kubwa iko kwenye hii ofisi. Watu wanauawa na inaporipotiwa, hakuna mtu anayejitokeza kuwa ni kweli watu wameuawa. Mali inaenda na watu wanaachwa bila chochote. Hakuna mtu anaangalia kwa nini hii mali inaenda. Hatupigani na watu wa kutoka mbali. Hivi ni vita vinavyotoka Kaunti ya Samburu. Naomba Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama na wenzake wachukue Ombi hili la Mhe. Lentoimaga na kulitilia maanani; walichukulie kuwa ni la ukweli na ni kitu kimeangamiza watu kwa muda mrefu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}