GET /api/v0.1/hansard/entries/941966/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 941966,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941966/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kuresoi North, JP",
"speaker_title": "Mhe. Moses Cheboi",
"speaker": {
"id": 329,
"legal_name": "Moses Kipkemboi Cheboi",
"slug": "moses-cheboi"
},
"content": " Mhe. Spika, niko na Kamusi nyingine ambayo nitampelekea ndugu yangu, Kiongozi wa Walio Wachache Bungeni. Nachukua nafasi hii kuwashukuru wale walio jumuika katika kazi hii. Ni kazi iliyofanywa kwa miezi sita. Kuna wafanyikazi wetu hapa waliofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba shughuli hii inafaulu. Pia, nashukuru Ofisi yako Bw. Spika kwa sababu wewe ndiye uliyetenga rasilimali za kuhakikisha kwamba tutakuwa Bunge la pili duniani kuwa na Kanuni za Kudumu zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Wafanyikazi hawa waliweza kutembelea Bunge la Taifa jirani la Tanzania ambalo lina Kanuni za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili. Ni wao peke yao waliokuwa na kanuni hizo kwa lugha ya Kiswahili duniani. Kwa hivyo, tutakuwa taifa la pili lenye Kanuni za Kudumu katika lugha ya Kiswahili Tumegundua kuwa Kiswahili cha Watanzania na chetu kina tofauti kiasi. Hii ndio sababu tumeamua kuwa hatutatumia kanuni hizi mara moja. Ni lazima zipigwe msasa. Najua wengi hawaelewi msasa ni nini. Ndugu yangu Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni atawaambia baadaye. Ni vyema tuwe na Kiswahili chetu cha hapa nchini. Tutahakikisha kuwa tumepeleka kanuni zetu katika vyuo vyetu vikuu hapa nchini kama Chuo Kikuu cha Nairobi ili wataalamu wa lugha wazipitie na kutupa nakala itakayokuwa ya hapa nyumbani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}