GET /api/v0.1/hansard/entries/941970/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 941970,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941970/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kuresoi North, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Moses Cheboi",
    "speaker": {
        "id": 329,
        "legal_name": "Moses Kipkemboi Cheboi",
        "slug": "moses-cheboi"
    },
    "content": " Mhe. Spika, ninawaelewa. Ni vigumu kuelewa lugha ya Kiswahili. Nilivyosema, Kiswahili ni lugha maskini. Kuna misamiati ambayo haipatikani kwa Kiswahili. Ni lazima uazime kutoka kwa lugha ya Kiingereza na utoe, kwa mfano neno \" Speaker\" ambalo ni la Kiingereza . Tukitafsiri \" Speaker\" kama \"Msemaji\" huko ni kupotoka; hicho si Kiswahili sanifu. Tukijaribu kutafsiri, tutapata shida kiasi. Kama ujuavyo, katika Bunge la Kitaifa, tuna Waswahili wa kutosha. Kwa mfano, kuna ndugu yangu niliyeketi naye hapa, ambaye ninashauriana naye. Anaitwa Mhe. Mwashetani. Kuna Waswahili wazuri Bungeni. Tuko na Mhe. Ali, Mjumbe Ali Wario, Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni ambaye amejifunza Kiswahili kama wengine na Captain Ruweida. Hili ni jambo la maana. Kuna lahaja za Kiswahili kama vile Kipate na Kiunguja. Kila mmoja wa wazungumzaji wake ana umahiri wa lugha. Naomba Wabunge waipitishe Hoja hii. Sababu ya kazi hii kufanywa haraka ni kuwa siku ya kesho – ambayo ni siku kubwa katika Bunge hili – tutakuwa na mkutano wa kwanza wa kuonyesha kamati za Bunge hufanya nini. Moja ya vitabu tutakavyozindua kesho ni Kanuni za Bunge la Taifa ambazo tunataka kupitisha siku ya leo. Kuna ndugu zangu kama Mhe. Kaluma na wengine ambao wamechoka kwa sababu hawaelewi. Kesho itakuwa siku nzuri. Tutazindua rasmi hizi kanuni. Mhe. Spika utafanya… Nimemshauri ndugu yangu ambaye amekaa karibu na mimi. Nitaomba ulinzi mwafaka kutoka kwako ili ndugu yangu aliye karibu nami anipe nafasi nimalize. Itakuwa vizuri Wabunge waje kwa wingi ili tuweze kuonyesha, kama Bunge, kuwa tuna kazi kadhaa ambazo sisi hufanya. Tunaongea Kiingereza na lugha ya taifa vizuri. Kuna kazi ambazo sisi hufanya ambazo hatuwezi kujipiga kifua, lakini kesho tutapata nafasi ya kueleza kuwa tunafanya kazi hizo. Lazima kesho tuonyeshe kuwa kamati ni za maana kama plenary. Mwenzangu ameniambia kuwa ni “ukumbi” kwa Kiswahili. Kwa hivyo, ni kama vile ukumbi wa Bunge unavyofanya kazi. Tuna shida kidogo na ndio sababu ya kuwa na kamusi hapa. Kwa Kiingereza tunasema “ The august House .” Nilimuuliza ndugu yangu ikiwa tafsiri yake tutasema ni “Nyumba ya Mwezi wa Nane”"
}