GET /api/v0.1/hansard/entries/941980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 941980,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941980/?format=api",
"text_counter": 252,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bura, JP",
"speaker_title": "Mhe. Ali Wario",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": " Mhe. Spika, leo ni siku ya furaha kwa hakika. Kwa heshima na taadhima kubwa, nachukua fursa hii kushukuru uongozi wa Nyumba, haswa akiwemo wewe, Katibu wa Kudumu wa Bunge na wafanyikazi wa Bunge kwa sababu leo wametupa tunu, wametupa zawadi, wametupa kitabu ambacho kwa mtazamo wa juu ukiangalia, watu watasema ni kitabu tu kama vitabu vingine. Lakini ili tutambue maana halisi ya kanuni za Bunge hili, Kifungu cha Saba cha Katiba na Kipengele 77 cha Kanuni za Bunge zinatambua Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya kitaifa katika nchi ya Kenya. Wengine tumeanza msafara mbali. Miaka 16 leo, utakapokwenda kwa kumbukumbu za Bunge la Taifa, utapata ni barua ngapi nimeandika, ni siku ngapi nimesimama ndani ya Nyumba nikidai na kuomba lini tutapata Kanuni. Kwa nini tunaomba Kanuni. Kwa uchache nikiguzia tu, Mau Mau walisema Mzungu aende Ulaya, Mwafrika apate Uhuru, uhuru wetu utabaki kamili lini wakati tunatumia lugha ya kigeni?"
}