GET /api/v0.1/hansard/entries/941983/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 941983,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941983/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bura, JP",
"speaker_title": "Mhe. Ali Wario",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": " Nashukuru Mhe. Spika. Kwa hivyo, Kiswahili si lugha geni. Kiswahili ni lugha yetu. Ili uhuru wetu ukamilike, mara kwa mara… Kwa ruhusa yako, nilikuwa kwa ofisi ya Kirui kujua amefikisha wapi hatua hii. Leo nina furaha kwa sababu ndio chimbukizo kwa utunzi wa sheria na sera kwa nchi nzima. Hivyo basi, ili tuweze kutunga sera na sheria kwa mujibu wa Kiswahili, ni lazima tuwe na kanuni za kudumu kwa Kiswahili. Tukio la leo ni la kihistoria. Mchakato mzima, msafara mzima wa kuleta Kanuni za Kudumu za Bunge la 12 la Kenya, unastahili kupewa kongole. Mimi leo kwa sababu ya furaha, sitaki kuzungumza kwa upana zaidi. Nimesimama kuafiki Hoja. Na naomba iweze kupitishwa leo ili kesho izinduliwe rasmi. Kwa hayo, nimesimama kuafiki. Ahsante."
}