GET /api/v0.1/hansard/entries/941991/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 941991,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/941991/?format=api",
    "text_counter": 263,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Garissa Township, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Aden Duale",
    "speaker": {
        "id": 15,
        "legal_name": "Aden Bare Duale",
        "slug": "aden-duale"
    },
    "content": " Mhe. Spika, inakubalika katika Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa kuangalia yale umeyaandika ukiongea na wenzako katika Bunge hili. Lakini bahali yake huyu mtu ni kusumbua watu. Bahali yake huyu Mheshimiwa wa Endebess ni mtu wa matata. Mimi nataka nipongeze na nishukuru Katibu wa Bunge la Kitaifa na lile Jopo ambalo lilitayarisha Kanuni hizi. Hii ni hatua muhimu sana katika historia ya Bunge hili na katika historia ya nchi yetu. Tutakumbukwa kama Wabunge waliowezesha kuwepo kwa Kanuni za Kudumu kwa Kiswahili. Na wewe pia utakumbukwa na Bunge la 12 litakumbukwa. Ni mara ya kwanza katika historia. Ningependa kuwaomba ndugu zetu Watanzania, kama wanatusikiliza na kufuatilia mjadala huu kwenye runinga, watusamehe. Huu ndio mwanzo wetu. Kadri tunavyoendelea, tutakuwa tumejua ufasaha wa lugha ya Kiswahili zaidi. Waheshimiwa wenzangu, Kiswahili ni sehemu ya maisha na utamaduni wa kila Mkenya."
}