GET /api/v0.1/hansard/entries/942006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942006,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942006/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Garissa Township, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Aden Duale",
    "speaker": {
        "id": 15,
        "legal_name": "Aden Bare Duale",
        "slug": "aden-duale"
    },
    "content": " Mhe. Spika, wahenga walisema, “Usiache mbachao kwa msala upitao.” Maana yake ni kwamba usiache ule mkeka wa zamani ukitafuta wa Kizungu. Hiyo ni kusema kwamba msala mbachao ni Kiswahili chetu. Kiswahili ni mbachao wetu. Kiswahili ni lugha yetu na ni sharti tukitukuze na kukienzi kama desturi yetu na pia kwa sababu Katiba yetu imetuamurisha kufanya hivyo. Mhe. Spika, watu wengi wako na shida ya lugha ya Kizungu. Hoja hii ya leo itawasaidia. Wale ambao hawajaweza kuongea tangu Bunge la Kenya lilipoanza kwa sababu kuzungumza Kizungu kwao imekuwa shida, leo tunawapatia fursa wasome Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa ili waweze kuleta Hoja. Wakitaka kuleta hoja ya kusema kwamba idadi ya Wabunge haijatosha, watasema hivyo kulingana ha hoja ya akidi ama “ lack of quorum ”. Kuna wengine wetu ambao hawajui maana ya “ quorum ”. Hao watasema “Hoja ya akidi”. Wale ambao hawajui “ Committee ” ni nini, watasema “kamati”. Taarifa ni “statement”. Ukitaka kuleta petition, utasema...Ninafundisha akina Mhe. Kaluma, Mhe. Mbadi, Mhe. T.J., Mhe. Junet, Mhe. Millie na wengineo. Kuna wenzetu ambao wanajua Kizungu lakini ikifika kuongea Kiswahili, wanazubaa, wanabaki mabubu kama watu ambao hawasikii. Kuna wenzetu katika Bunge hili ambao Mhe. Mbadi, Mhe. T.J na Mhe. Shollei wanapozungumza Kizungu, wanakua mabubu. Sasa kuna fursa ya Bunge hili kujaa. Kila mtu anaweza kuongea Kizungu ama Kiswahili. Tukiendelea mbele, tutaleta lugha ya mama pia kwa sababu kuna wenzetu ambao hawajui Kiswahili ama Kizungu. Uongozi si lugha; uongozi ni vitendo. Uongozi si vile unavyoongea katika Bunge hili. Mhe. Spika, jina lako litaingia kwenye kumbukumbu za historia. Ni katika enzi yako ambapo tuliweza kupata hiki chombo cha kupigia kura. Leo pia, umekalia Kiti cha Spika wakati tunapitisha Hoja hii. Kenya ni nchi ya pili ulimwenguni kupitisha Kanuni za Bunge za Kudumu. Mhe. Spika, wengine wetu tutaandika vitabu na tutakupatia sura rasmi yako kama Spika ambaye ameleta mabadiliko muhimu katika Bunge. Wale wa zamani hawakufanya hivyo lakini walijaribu."
}