GET /api/v0.1/hansard/entries/942018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942018,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942018/?format=api",
    "text_counter": 290,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mbunge Mteule, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. (Bi.) Dennitah Ghati",
    "speaker": null,
    "content": "Kanuni hizi ambazo zitaingia Bunge zitasaidia ili tuweze kuelewa vyema jinsi ambavyo tunajadiliana katika Bunge hili. Ninapoongea hivyo, ningeomba kwamba tunapoendelea kutumia lugha ya Kiswahili katika Bunge hili, wewe ukiwa kama Spika wetu, ningependa kuleta hoja ya kwamba katika siku hizi tatu ambazo tuko katika Bunge hili, ambalo tunaliita august House, uitenge siku moja ili Wabunge wenzetu waongee kwa lugha ya Kiswahili. Tukifanya hivyo, tutahakikisha kuwa tunakuza lugha ya Kiswahili."
}