GET /api/v0.1/hansard/entries/942023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942023,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942023/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mbunge Mteule, ODM",
"speaker_title": "Mhe. (Bi.) Dennitah Ghati",
"speaker": null,
"content": "Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni alianza kwa kuongea Kiswahili. Tunaona kwamba Wabunge wenzetu wanazidi kutoka nje kumaanisha kwamba wanaogopa Kiswahili. Unaona wanachomoka mmoja baada ya mwingine. Kwa hivyo, ili tuhakikishe kwamba Kiswahili kinatumika jinsi ambavyo Katiba ya Kenya imekitambua, iwe ni lugha ambayo inaweza ikaongelewa katika Bunge la Kitaifa. Kwa hivyo, kesho wakati utakapokuwa unazindua hizi Kanuni za Kudumu katika Bunge hili la Kitaifa, ningependa kuomba hivi: Kwa vile tumeketi hapa, ninakuomba kila Jumatano asubuhi ama mchana wakati ambapo tuko na kikao katika Bunge hili, iwe ni siku ambayo tunajadiliana katika Bunge hili kwa lugha ya Kiswahili."
}