GET /api/v0.1/hansard/entries/942026/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942026,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942026/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ugenya, MDG",
    "speaker_title": "Mhe. David Ochieng’",
    "speaker": {
        "id": 2955,
        "legal_name": "David Ouma Ochieng'",
        "slug": "david-ouma-ochieng"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Nina furaha sana nikiunga mkono Hoja hii ya kuleta Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa. Lugha ya Kiswahili ni muhimu sana na Katiba imeitambua kama lugha ya kitaifa pamoja na lugha ya Kiingereza. Jumuiya ya Afrika Mashariki inatumia lugha hii ya Kiswahili. Kiswahili kinafudishwa katika shule za msingi, sekondari na hata vyuo vikuu. Leo hii ni jambo la busara kwa sababu Wabunge wamekubaliana na aliyeleta Hoja hii kwamba Kiswahili ni lugha tunayotumia tukitafuta kura. Pia ni lugha ya mama kwa kila mtu mtaani. Kwa hivyo, tukipitisha hizi Kanuni, Wabunge wote hata mimi ni lazima tujue kuzitumia. Hili ni jambo ngumu sana kwa sisi Wabunge wa Kenya. Ukiwasikia Wabunge wa Tanzania wakiongea lugha ya Kiswahili, inapendeza. Lakini aliyeleta Hoja hii amesema kwamba sisi kama Wakenya pia tuwe na Kiswahili chetu. Sio lazima tuzungumze Kiswahili safi kama Watanzania. Tunaweza kuwa na lugha yetu kama Sheng ambayo ni lugha ya mtaa. Kwa hivyo, Mhe. Spika, ningependa utuelekeze vile tutakuwa na Kiswahili chetu ambacho kitaeleweka na Wakenya na Watanzania ama Waganda hawataelewa matamshi fulani. Ukienda Tanzania, wanaongea Kiswahili shupavu lakini hapa Kenya, tuna Kiswahili chetu. Pia Uganda wako na Kiswahili chao. Ndiyo nakubaliana na Naibu Spika kwamba kama Wakenya tuwe na Kiswahili chetu ndiyo tukizungumza hapa Bungeni, hata wananchi wanaelewa. Tusiongee Kiswahili cha ndani sana kama cha Mwashetani ama Wario, lakini kile rahisi cha mtaani ambacho kila Mkenya ataelewa. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii na kuwaomba wenzangu wauunge mkono. Ahsante sana Mhe. Spika."
}