GET /api/v0.1/hansard/entries/942028/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942028,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942028/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lungalunga, JP",
"speaker_title": "Mhe. Khatib Mwashetani",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Mwanzo nakushabikia sana. Wabunge wenzangu waliotangulia kunena wamesema kwamba utaingia katika historia na kumbukumbu kwa vile umekipa nguvu Kiswahili. Umehakikisha katika mipango yako yote umekiweka katika usikizano na kueleweka na Wabunge watakaokuwa wakiongea lugha hii. Kiswahili ni lugha yetu na ni lazima tuwe na madaha nayo. Tukisikia wenzetu wanavyozungumza kwenye Bunge la Kitaifa la Tanzania, sio kuwa hawakusoma. Ile fikira kwamba anayezungumza Kiswahili hakusoma ni fikira ya uongo. Kwa sababu lazima tutambue kuwa kuna zile lugha ambazo zimekuja na zile tuko nazo. Wabunge wote ndani ya Bunge la The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}