GET /api/v0.1/hansard/entries/942029/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942029,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942029/?format=api",
"text_counter": 301,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lungalunga, JP",
"speaker_title": "Mhe. Khatib Mwashetani",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "Kitaifa ama Seneti tukitafuta kura, tunatumia lugha ya Kiswahili. Lakini Kiswahili kile ni lugha ambayo kidogo hatujaipatia nguvu. Kwa wale Wabunge ambao wako hapa, niko na imani kwamba wakipatiwa fursa ya kuzungumza Kiswahili, kila mmoja anaweza kuzungumza. Kama vile Mhe. Dennitah alivyotangulia kusema, itakuwa ni vizuri kama Kiswahili kingepatiwa nafasi katika zile siku nne tunazoketi katika Bunge hili la kifahari. Ndiyo tuwe na kikao kimoja ambacho Wabunge watajadili kwa lugha ya Kiswahili ili wawe na motisha na kila Mbunge atajitahidi kwa vyovyote kuzungmza hii lugha. Sisi tunaotoka Pwani, kila siku tunawasiliana na wananchi wetu. Kuna Hoja zingine ambazo zinaletwa hapa zikiwa na maneno mengine ambayo yameombwa kutoka kwa lugha ya Kiingereza. Kama ukizungumza kwa lugha ya Kiswahili upande wa fedha, utapata neno kama \" appropriation\" ambalo haliko katika lugha ya Kiswahili. Ukiambiwa kwa Kiswahili kwamba mace inaitwa siwa, wengi tutapotea. Pia kusoma dondoo ni \" refer\" . Haya maneno yote yatakuja pole pole. Niko na imani na motisha na nguvu ambazo umetupatia. Pia niko na imani Wabunge watazungumza Kiswahili sanifu. Ila tu katika hizi Kanuni za Kudumu ambazo leo tunazijadili, nina imani kuwa Wabunge wote watapitisha Hoja hii ili kesho tuweze kuzipeana ziwe za kutumika katika Kikao cha Nne cha Bunge hili la Taifa. Mimi kama Mbunge wa Lungalunga nimekuwa nikizungumza Kiswahili hapa Bungeni. Lakini sio kuwa nimekamilika kwa Kiswahili. Kiswahili ni kama Kizungu kwa sababu bila kukizungumza, kitakutatiza. Pia bila kuzungumza Kiswahili, kitakutatiza. Sisi katika Bunge hili, hii si mara ya kwanza. Hii ni lugha ambayo tayari Katiba imeitambua na Kanuni zetu zimeitambua katika Kanuni ya 77 ambayo inampa Mbunge yeyote ruhusa kujadili maswala ya Bunge akitumia lugha ya Kingereza au Kiswahili. Lazima umalizie katika ile lugha ulianzia. Hii basi tayari inaonyesha kuwa Katiba imetambua Kiswahili kama lugha ya taifa. Basi sisi tunaipa nguvu leo ili tuweze kutumia maneno sawasawa katika lugha hii. Mhe. Spika nasema ahsante kwa kunipatia fursa hii. Nawaomba Wabunge wezangu waunge mkono Hoja hii ili tuwe Bunge la pili katika dunia kukipatia nguvu Kiswahili. Hii ni kwa sababu hata katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ukiangalia Rwanda, tayari wameanza, Tanzania wamekamilika. Basi hata sisi hatutakuwa pabaya ikiwa tutakamilisha kwa kusema tuwe na nafasi moja katika vikao vinne kuzungumza Kiswahili. Ahsante sana Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii."
}