GET /api/v0.1/hansard/entries/942038/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942038,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942038/?format=api",
    "text_counter": 310,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Suba North, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. (Bi.) Odhiambo-Mabona",
    "speaker": {
        "id": 376,
        "legal_name": "Millie Grace Akoth Odhiambo Mabona",
        "slug": "millie-odhiambo-mabona"
    },
    "content": "Mhe. Spika, ningeomba unilinde dhidi ya wale wanacheka bila kunyamaza. Jukumu letu ni kuhakikisha kuwa Wakenya wanafahamu yale tunasema Bungeni. Ndio sababu nasema ingefaa tutafsiri kwa Sheng . Nataka pia kupongeza Wanyarwanda kwa sababu tayari wameongeza Kiswahili kama lugha ya taifa. Ningeomba pia Kenya tuongeze Kifaransa ndio sasa tutakuwa na kile kitu kinaitwa Pan Africanism . Hawa wengine wanajifanya wanajua Kiswahili sasa wajaribu kutafsiri Pan Africanism. Najua hawajui. Mhe. Spika, ingawa tunaongea kuhusu Hoja ya Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa, tusisahau kuzuia mmomonyoko wa ardhi. Tusifanye tu leo lakini tufanye kesho, kesho kutwa, mtondo na mtondogoo. Nilikuwa nataka kuwaeleza hawa kuwa naelewa Kiswahili. Kwa hayo machache, naunga mkono. Ahsante, Mhe. Spika."
}