GET /api/v0.1/hansard/entries/942040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942040,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942040/?format=api",
"text_counter": 312,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mbunge Mteule, JP",
"speaker_title": "Mhe. David ole Sankok",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Naelewa kwamba “Bwana Spika” kwa lugha rasmi ya Kiswahili ni “Kiranja wa Bunge”. Nashukuru kwa fursa hii ambayo umenipatia niunge mkono Hoja hii. Mhe. Spika, nakupongeza. Kama watangulizi wangu walivyosema, utaingia katika vitabu vya kumbukumbu kwamba wewe umeleta maneno mazuri katika Bunge la 12. Umeleta vifaa hivi ambavyo tunasema ni vya kidijitali. Pia umeleta Kanuni za Kudumu katika Bunge hili. Kabla hujaleta, mimi nilikuwa nafikiri Standing Orders zinaitwa “amri ya kusimama”. Lakini sasa nimejua haziitwi hivyo. Wabunge wenzangu wakistaajabu ya Musa, wataona ya Firauni. Ya Firauni bado yaja kwa sababu katika nchi hii, tuko na lugha tatu ambazo zinafahamika kama lugha za taifa. Lugha hizo ni Kiswahili, Kiingereza na Lugha ya Ishara ya Kenya. Mimi ningetaka pia wakati ambao tutasema Jumatano asubuhi tutaongea kwa lugha ya Kiswahili, basi saa nane tuongee Lugha ya Ishara ya Kenya. Kwa wale ambao hawajui, Lugha ya Ishara ya Kenya ni Kenya Sign Language . Hii inatambulika kama lugha ya tatu katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo, ikifika Jumatano saa nane Mhe. Spika nakuomba kila mtu anyamaze. Hakutakuwa na kelele. Itakuwa…"
}