GET /api/v0.1/hansard/entries/942046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942046,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942046/?format=api",
    "text_counter": 318,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mbunge Mteule, JP",
    "speaker_title": "Mhe. David ole Sankok",
    "speaker": null,
    "content": "kuongea Kiswahili sanifu. Ndio sababu nimefanya hivi kwa sababu unampatia sign name . Ndio sababu nilikuwa narefer kwake. Kwa hivyo, Mhe Spika, nakuomba kwa sababu Kenya imetambua lugha tatu, pia tutambue, kama Bunge, lugha zote tatu kwa sababu hakuna wakati ambapo wenzetu ambao wako na ulemavu wa kutosikia wanajua chenye tunazungumza hapa ndani ya Bunge. Wakiona wengi wetu kama mimi, Mhe. Junet na Mhe. Mbadi ambao tunaongea tukirusha mikono kama tuko katika mkutano wa hadhara, wanafikiri tunapigana ndani ya Bunge kwa sababu hawaskiii chenye tunasema. Na hao ni milioni moja katika nchi ya Kenya. Pia ni wananchi ambao walitupigia kura na wanataka kujua chenye kinaendelea katika Bunge hili. Mhe. Spika, nakuomba kwa unyenyekevu mkubwa sana kwamba pia tutambue lugha hiyo na wakati ambapo tutakuwa na live coverage kesho, iwe na lugha ya ishara pia ili waweze kufuata. Nimefurahi sana wakati huu ambao niko Bunge la 12 kuona kwamba tutakuwa tukiongea Kiswahili sanifu. Umesikia nikiongea Kiswahili sanifu. Nimeongea vizuri kuliko Mhe. Millie Odhiambo. Wenye wamenipita ni Spika na Naibu Spika peke yao. Nimemshinda Mhe. Mbadi na hata Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi. Kwa hivyo, leo nimejaribu na inaeleweka sasa kwamba sisi Wamaasai tunatangatanga kwa lugha ya Kiswahili kuelewa kabisa. Sisi hatujui kungoja kueleweka baadaye ama kutoeleweka. Sisi tumeshatangatanga ndani ya lugha ya Kiswahili kikamilifu tukiwa Wamaasai na wafugaji wote tuko na Kiswahili kabisa. Ahsante sana na naunga mkono Hoja hii mia kwa mia."
}