GET /api/v0.1/hansard/entries/942050/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942050,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942050/?format=api",
"text_counter": 322,
"type": "speech",
"speaker_name": "Suba East, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Junet Nuh",
"speaker": {
"id": 2840,
"legal_name": "Junet Sheikh Nuh",
"slug": "junet-sheikh-nuh"
},
"content": "Siwezi kukuambia ati nitaongea dakika tano. Nitakuwa nakudanganya. Nitaongea dakika mbili peke yake. Jambo la kwanza ni kushukuru Bunge kwa kutafsiri Kanuni hizi kwa Kiswahili. Namshukuru pia Naibu Spika. Neno “Spika” ni la Kiingereza. Nimewazia jinsi linaweza kugeuzwa kuwa Kiswahili. Sijui kama nitakosea kwa kusema liwe ‘Mstahiki Mkurugenzi wa Bunge’. Nataka neno hilo liwekwe kwenye gazeti kama watu watakubali. Naishukuru Bunge kwa sababu hili ni jambo muhimu sana. Kuna wakati nilimsikia Mbunge mwenzangu akisema kuwa kuna wale wanaoongea Kiingereza kingi huko Bunge. Sasa watu waje waongee Kiswahili kingi hapa Bunge. Hakuna haja ya Kiingereza. Lugha hii siyo vile tunavyofikiria. Wakati unapoongea katika matanga ama rally, unaongea Kiswahili lakini hujui unasema nini. Kumbe kuongea lugha hii hapa na huko nje ni tofauti. Kuna maneno muhimu ambayo lazima uzungumze. Jambo hili limechelewa. Lilifaa lije zamani. Unapaswa uangalie vile wanavyozungumza katika Bunge la Tanzania. Hapa Bungeni kuna aina tofauti tofauti za watu. Kuna wasomi, wale wamesoma sheria, madaktari na wakulima. Sasa wakulima na wezi wa ng’ombe wanaweza kuongea Kiswahili. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}