GET /api/v0.1/hansard/entries/942053/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942053,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942053/?format=api",
    "text_counter": 325,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mosop, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Vincent Tuwei",
    "speaker": {
        "id": 13436,
        "legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
        "slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bwana Spika kwa kunipa nafasi au fursa hii ili nichangie jambo hili ambalo ni la kuleta raha, furaha, basheshe na bashasha. Hiyo ni lugha ya Kiswahili. Nataka kukupongeza kwa sababu utakuwa katika kumbukumbu za vitabu vya Bunge kama aliyeleta mabadilisho - that is reforms - ambayo tumeyaona katika Bunge hili la 12. Nakushukuru kwa sababu lugha ya Kiswahili ina lahaja mbali mbali. Mimi kama Mkalenjin kutoka Nandi, tuko na lahaja za Kinandi. Mjaluo pia ako na lahaja zake za Kijaluo. Wale ambao wanaongea lugha ya Kiswahili kutoka Pwani si kwamba hawana lahaja katika lugha hii. Nashukuru kwa sababu tumezindua Hoja ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili sisi sote tupate kujumuika katika hali ya kuchangia na kukuza lugha hii ili ikubalike Afrika Mashariki na ya Kati. Ndugu wapenzi, Wabunge wenzangu, lugha hii si ngumu kuelewa. Siku ikitengwa maalum ya kuchangia katika lugha ya Kiswahili, sisi sote tutaenda maabarani kuangalia vizuri ni lugha gani na msamiati gani tutatumia. Niko na kitabu ambacho Waswahili na wale ambao wanaongea lugha ya Kiswahili na ya King’eng’e wamejaribu kuidhalilisha ili tuipate katika lugha ambayo inafaa. Inaitwa Istilahi za Kiswahili. Hapo ndipo tunaweza kupata mambo yanayohusiana na Kizungu ili tuchangie Miswada na Hoja ambazo tutapata hapa Bungeni. Nashukuru sana kuona Mheshimiwa Junet anajikakamua kabisa kuelewa lugha ya Kiswahili kwa njia zote. Kupotea njia ndio kujua njia. Kutoka leo, tukianza kuongea lugha hii ambayo tunaienzi na kuipenda wakati tunapata nafasi ya kuchangia Miswada na maono yetu, tutaongea kwa wepesi na kuizoea zaidi. Kumalizia ni kwamba lugha ya Kiswahili inakua. Kuna maneno ambayo tutaazima kutoka lugha nyingine kama Kizungu na lugha inayohusiana na kitaalamu. Wataalamu wengine kama madaktari wako na lugha yao. Tunaweza kuchukua kutoka kwa lugha yao katika ile hali ya kujieleza. Nashukuru kwamba mwaka huu tutaongea lugha ambayo itakuwa rahisi kwa wananchi ambao tunawaongoza kuelewa ni nini ambacho tunasema kama Wabunge. Sheria ikitungwa katika lugha ambayo wananchi wanaelewa, ni rahisi kwao kufuatilia maelezo, matukio na maendeleo hapa Bungeni. Ili nisichukue muda mrefu, nachukua nafasi hii kukupongeza na kushukuru wenzangu na wale wote ambao wamefanya ukalimani na kutafsiri hizi Kanuni za Kudumu katika lugha ya Kiswahili. Nawapongeza sana. Tukae tukijua kwamba lugha ya Kiswahili inakua siku baada ya siku. Kwa hayo machache, nashukuru kwa nafasi na fursa ambayo nimepata kuchangia wazo hili."
}