GET /api/v0.1/hansard/entries/942057/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942057,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942057/?format=api",
"text_counter": 329,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitui Central, WDM-K",
"speaker_title": "Mhe. Makali Mulu",
"speaker": {
"id": 1955,
"legal_name": "Benson Makali Mulu",
"slug": "benson-makali-mulu"
},
"content": " Ahsante sana, Mheshimiwa Spika. Ningependa kujiunga na wenzangu kuunga mkono Hoja iliyo mbele ya Bunge hili. Siku ya leo, tumeandika historia kama Bunge la 12. Ukiangalia Katiba yetu, tuliidhinisha kama Wakenya kuwa Kiswahili kitakuwa lugha rasmi ya nchi yetu. Itatubidi tutie bidii ili tuweze kuongea lugha hiyo rasmi. Kwa hivyo, ninapoona Kamati husika ikitia bidii tuweze kupata hizi Kanuni za Kudumu, lazima tuipongeze kwa sababu imefanya kazi nzuri. Sisi kama Wabunge, hatuna budi ila kusema pongezi sana. Kama Mbunge wa sehemu za mashambani, nafurahi sana tunapoongea lugha ya Kiswahili kwa sababu nina uhakika kwamba mzazi wangu ambaye haelewi Kiingereza, wakati mwingine atapata kusikia na kuelewa. Kwa hivyo, Mhe. Spika, tunapojitayarisha ili siku zijazo tuweze kuanzisha Kanuni za Kudumu rasmi, kama Wabunge wa Bunge la 12, tunafurahi sana. Tulisoma Kiswahili na tulipomaliza kidato cha nne, hatukuendelea zaidi ya hapo. Lakini, ninaamini kwamba tutatia bidii ili tuweze kuongea Kiswahili. Ninashukuru sana kwa sababu wale wote ambao wako na tatizo la kuongea Kiswahili kidogo, kama Mhe. Millie Odhiambo na wengineo, wanatia bidii. Ni vizuri tuendelee kutia bidii."
}