GET /api/v0.1/hansard/entries/942068/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942068,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942068/?format=api",
"text_counter": 340,
"type": "speech",
"speaker_name": "Turkana Central, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Lodepe Nakara",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Pili, tutakuwa tunatia watu wetu morale ya kutazama runinga waone vile ambavyo tunaongea. Watu wetu watakuwa wakitazama runinga nyumbani waone vile waheshimiwa wanajadili mambo ya taifa kwa sababu wengine hawajui Kiingereza. Tutakapokuwa na siku moja ya kujadili Hoja zetu kwa lugha ya Kiswahili, tutawapatia watu wetu morale ya kutazama runinga ili wafurahi. Naona ya kwamba jambo hili ni nzuri. Mhe. Spika, kama walivyosema wenzangu, jina lako litaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mmoja wa Waheshimiwa Spika katika Bara la Afrika waliotafsiri Kanuni za Kudumu za Bunge la Taifa kwa lugha ya Kiswahili."
}