GET /api/v0.1/hansard/entries/942075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942075/?format=api",
"text_counter": 347,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru CWR, JP",
"speaker_title": "Mhe. (Bi.) Liza Chelule",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Nimekuwa nikijua ya kwamba Kiswahili siyo lugha rahisi sana. Kuongea Kiswahili sanifu ni kazi ngumu sana. Kukubali kama taifa la Kenya kutumia Kiswahili katika Bunge letu ni kwa maana sana, sio kwa Wabunge peke yao lakini kwa wale wote waliotuchagua kule nyumbani. Unaelewa kwamba wengi ambao walituchagua ni zaidi ya asilimia 90 ama 80. Kwa hivyo, tukianza kutumia Kiswahili ndani ya Bunge, watafurahi sana na watakuwa wakitenga wakati kusikiza kwa umakini ni nini tunaongea. Mambo ambayo tunaongea mara nyingi ni yale yanayohusu wananchi wa Kenya, na wengi wao hutumia Kiswahili."
}