GET /api/v0.1/hansard/entries/942076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 942076,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942076/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru CWR, JP",
"speaker_title": "Mhe. (Bi.) Liza Chelule",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Mhe. Spika, nimefurahi sana kwa kuanza kutumia Kiswahili. Tunakupongeza. Ninampongeza Mhe. Naibu Spika ambaye alijaribu sana kuitetea Hoja hii wakati aliposimama kuongea kuhusu kuzinduliwa kwa matumizi ya Kiswahili katika Bunge hili. Nawapongeza sana. Nampongeza Mhe. Millie sana kwa sababu alijaribu sana kuongea kwa lugha ya Kiswahili. Kama ulivyosema, ni heri tupatiwe nafasi tuchanganye lugha ya Kiswahili na Kiingereza wakati huu tunapoanza. Ikiwa huwezi kutamka neno fulani kwa Kiswahili, unaweza pia kulitamka kwa Kiingereza. Tutaendelea kujua kuzungumza Kiswahili. Kama leo, nimejua maana ya neno “dondoo”. Kwa hivyo, kutumika kwa hii lugha katika Bunge letu ni bora sana. Nafurahi na ninajua tutajifunza sisi sote. Unaelewa kwamba kuna sehemu fulani humu nchini ambako watu hawakujifunza Kiswahili darasani. Nilipata bahati kwa sababu kwetu tulikuwa tukifunzwa Kiswahili kutoka darasa la kwanza hadi darasa la saba. Kuna watu wengine ambao hawakujifunza na hii itakuwa ni nafasi yao ya kujifunza ili twende mbele pamoja. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya maana sana, kwa sababu akina mama kule nyumbani wataelewa ni nini tunazungumzia hapa Bungeni. Wengi wao hawaelewi Kiingereza. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}