GET /api/v0.1/hansard/entries/942080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 942080,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/942080/?format=api",
    "text_counter": 352,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Seme, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. (Dkt.) James Nyikal",
    "speaker": {
        "id": 434,
        "legal_name": "James Nyikal",
        "slug": "james-nyikal"
    },
    "content": " Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii nichangie mjadala wa Kanuni za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni Hoja muhimu sana kwa sababu kulingana na Katiba yetu, tuko na lugha tatu za kitaifa, kama Kizungu, Kiswahili na Lugha ya Ishara ya Kenya. Ni vizuri tutumie lugha zote hasa Bungeni ambapo mambo yote ya kitaifa yanajadiliwa. Tuko kwa Jumuia ya Afrika Mashariki na hatuwezi kusema kuwa hatuwezi kutumia lugha hizi. Tukienda kwa Bunge la Afrika Mashariki ni lazima tutumie lugha ya Kiswahili. Sio hapo peke yake. Shuleni, watoto wanafunzwa Kiswahili. Sio vyema kutumia pesa kukifunza Kiswahili ilihali hatukitumii Bungeni. Ni muhimu tufanye mazoezi ya kutumia lugha ya Kiswahili ili tuzoee kuitumia. Nchi zingine kama Korea, Japan ama Uchina wanatumia lugha zao kwa sayansi. Kwa hivyo ni lazima tukikuze Kiswahili hata tuandike vitabu vya sayansi ama vya uuguzi kwa lugha ya Kiswahili. Hivyo tutaendelea. Siku ya leo ni muhimu sana kwa kuidhinisha Kanunu za Kudumu kwa Lugha ya Kiswahili. Mhe. Spika, tuchape vitabu vingi kwa lugha ya Kiswahili. Kama vile Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni amesema, kila Mbunge apewe Kamusi ili tujifunze na tuendelee kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili Bungeni na shuleni. Tutakuza Kiswahili hivyo ili tukitumie kama lugha yetu ya taifa. Asante sana, Mhe. Spika. Ninaunga Hoja hii mkono."
}